Science of Mind Africa
Change Your Thinking. Change Your Life.
Science of Mind Africa welcomes people from all backgrounds, faiths, cutures, and spiritual paths. We believe that beneath our many different traditions is a universal spiritual truth that can inspire, empower, and transform the way we experience life.Our vision is to contribute to a more conscious, compassionate, and empowered world—one person at a time.We support individuals on their journey of self-discovery, personal empowerment, and conscious living by helping them develop greater awareness, practice gratitude, and make intentional choices about the life they want to create.Through mindful practices, spiritual principles, and practical tools for everyday life, we create opportunities for people to awaken their inner potential, deepen their understanding of themselves, and create meaningful change from the inside out.We believe that our outer experience of life is deeply influenced by our inner world. As we become more conscious of our thoughts, beliefs, attitudes, and choices, we begin to open the door to new possibilities.When we change the way we think, we change the way we see ourselves, others, and the world around us—and ultimately, we change the way we experience Life.
One of our on Going Classes
SPIRITUAL ECONOMICS — ERIC BUTTERWORTH
Spiritual Economics ni kitabu cha Eric Butterworth kinachotualika kubadilisha mtazamo wetu kuhusu pesa, utajiri, mafanikio na maisha ya wingi.
Butterworth anatufundisha kwamba utajiri wa kweli hauanzi na kiasi cha pesa tulicho nacho, bali huanza na mawazo na mtazamo tulio nao kuhusu pesa na uwezo wetu wa kuumba maisha tunayoyataka.
Kitabu hiki kinatufundisha kuondoka katika fikra za upungufu, hofu na kukosa, na kuanza kutambua kwamba kuna wingi wa kiroho na fursa nyingi ndani yetu na katika maisha yetu.
Badala ya kuona pesa kama kitu cha kuogopwa au kuabudiwa, tunajifunza kuiona kama chombo kinachoweza kutumika kwa hekima, huduma na kujenga maisha yenye maana.
Eric Butterworth anatukumbusha kwamba:
“Utajiri huanza ndani kabla haujaonekana nje.”
Huduma Ambazo Tunatoa
Programu zetu huwasaidia watu barani Afrika kuyaelewa na kuyatumia mafundisho ya Science of Mind katika maisha yao ya kila siku. Tunafanya hivyo kupitia madarasa ya bure, kutafsiri mafundisho ya New Thought, kambi za vijana, ufadhili wa masomo, na vituo vya jamii vinavyokuza ufahamu.
Madarasa ya Science of Mind na Mafunzo ya Wataalamu wa Kiroho
SOMA hutoa madarasa ya bure na yaliyoidhinishwa ya Sayansi ya Akili (Science of Mind) pamoja na vifaa vya kujisomea kwa wanafunzi, kwa lengo la kumsaidia kila mtu kuamsha ukamilifu alio nao ndani yake na uwezo wake wa kiungu.
Kupitia madarasa ya mtandaoni na vikundi vya masomo vinavyoandaliwa kulingana na mazingira ya maeneo husika, wanafunzi hushiriki katika mazoea ya kina ya kiroho, yakiwemo Sala ya Uthibitisho (Spiritual Mind Treatment), Kuona kwa Maono (Visioning), Kutafakari (Meditation), na Msamaha (Forgiveness).
SOMA pia huwasaidia wanafunzi kwa kuwapatia ufadhili na kuwaongoza kupitia Shule ya Uongozi ya CSL (Mafunzo ya Ualimu wa Kiroho) pamoja na Mpango wa Uongozi wa Jamii wa CSL, ili kuwajengea uwezo wa kuwa viongozi na walimu wa kiroho katika jamii zao.
Tafsiri za Kiswahili na Maktaba ya Kukopesha Vitabu
Tunaamini kwamba hakuna mtu anayepaswa kutengwa na hekima ya kiroho kwa sababu ya lugha. SOMA imetafsiri vitabu na maandiko mbalimbali, pamoja na muziki wa New Thought, na kuandaa rasilimali za sauti na kidijitali kwa Kiswahili, ili kuondoa kikwazo cha lugha na kuwafikia watu kote Afrika.
Kiswahili ni mojawapo ya lugha zinazozungumzwa kwa mapana zaidi barani Afrika, na hutumika kama lugha ya mawasiliano kwa zaidi ya watu milioni 200. Pia tumeanzisha maktaba ya mtandaoni ya kukopesha vitabu kwa Kiswahili, ili watu wengi zaidi waweze kupata na kusoma vitabu na rasilimali za kiroho kwa urahisi.
Kambi za Uongozi kwa Vijana
Vijana wa leo ndio watakuwa wabunifu na viongozi wa mabadiliko ya kesho, wakiwa na ufahamu na uelewa mpana.
SOMA huandaa kambi za mabadiliko kila mwaka: “Free to Be Me” kwa wasichana matineja na wanawake vijana (miaka 13–18), pamoja na “Woke Mtaa” kwa vijana wa kiume (miaka 19–26).
Washiriki hujifunza kutambua thamani na uwezo wao wa asili, kujifunza njia za kutatua migogoro bila kutumia vurugu, kuchunguza Mchakato wa Uumbaji (Creative Process), na kujenga mitandao ya marafiki na wenzao inayowasaidia na kudumu kwa muda mrefu.
Programu hizi huendeshwa chini ya mwongozo wa Wataalamu wa Science of Mind wenye leseni na walezi (mentors), wanaowasaidia vijana kukua katika uelewa wao binafsi, kiroho na kijamii.
Watu Halisi. Mabadiliko Halisi.
Pata kuelewa jinsi Sayansi ya Akili Afrika Imeweza kubadili maisha ya baadhi ya wanachama
“Mawazo sahihi huzaa matokeo sahihi. Science of Mind ilibadilisha namna ninavyoongoza, ninavyotoa, na ninavyoamini katika riziki na utele wa Mungu. Baada ya kutumia Mchakato wa Uumbaji katika kazi yangu, ufanisi wa timu yetu uliongezeka kutoka 45% hadi 65% ndani ya mwezi mmoja tu. Wakati huo huo, nilitimiza 100% ya ahadi yangu ya kutoa kwa kanisa — na kipato changu binafsi kikaongezeka kwa 50%. Kanuni hizi hazikubadilisha tu matokeo yangu. Zilibadilisha ufahamu wangu.”
“Kabla ya kujifunza Sayansi ya Akili, nilihisi kana kwamba maisha yalikuwa yananitokea tu na sikuwa na uwezo wa kuyaongoza. Mafundisho haya yalinionyesha kwamba Akili ile ile yenye Hekima inayoendesha ulimwengu inaishi ndani yangu — na kwamba mawazo yangu yana nguvu halisi ya kuumba.
Hayakunipa dini mpya. Yalinipa uhusiano mpya na Mungu, na maisha, na nafsi yangu.”*
“Nilijiunga na SOMA mwezi Januari 2026, na jambo ninalolipenda zaidi ni jinsi ilivyo wazi na inayomkaribisha kila mtu anayechagua kushiriki katika programu mbalimbali.
Kuanzia madarasa yanayotolewa, mikusanyiko ya kijamii, miduara ya wanawake na wanaume, hadi programu za vijana, vijana balehe na watoto, familia nzima inahudumiwa kwa ukamilifu.
Ni furaha kubwa kuweza kushiriki kama familia na kuendelea kuishi na kutekeleza kwa pamoja falsafa ya Science of Mind. Natarajia kukua zaidi kiroho na kusaidia kueneza mafundisho haya yanayobadilisha maisha kote nchini Kenya na Afrika.”*
Baadhi ya Mikutano yetu
Picha hizi ni baadhi ya Mikutano yetu barani Afrika







